BAADA ya kufunga bao pekee ambalo limepeleka ushindi kwa timu yao dhidi ya Mbeya City jana, Straika wa kikosi cha Azam, Idriss Mbombo ameahidi kufanya vizuri zaidi msimu huu.

Mchezo huo wa ligi uliokutanisha timu hizo ulipigwa jana jumanne kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya ambapo Azam walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 likifungwa na Mbombo.

Mbombo, Mbombo Aahidi Jambo, Meridianbet

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mbombo alisema kuwa: “Kwanza namshukuru Mungu kwa kumaliza salama mchezo na kuipa ushindi timu yangu.

“Mchezo ulikuwa mgumu lakini kocha alitupa maelekezo tukayafuata na
tumefanikiwa kupata pointi tatu.

“Ninachowaahidi mashabiki wa Azam kwa msimu huu ni kufanya vizuri zaidi na kuisaidia timu kutimiza malengo yake alafu malengo yangu yatakuwa baada ya timu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa