Ben White Aongeza Kandarasi Arsenal

Beki wa kulia wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza Ben White amefanikiwa kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mingine minne.

Ben White moja ya wachezaji ambao wamekua wakionesha ubora mkubwa ndani ya kikosi cha Arsenal, Ikiwa ndio sababu ya wahika mitutu hao wa London kuhitaji kuendelea kua na beki huyo.ben whiteKlabu ya Arsenal wamekua wakiwaongezea wachezaji wake ambao wana umri mdogo mikataba kwajili ya mipango mikubwa zaidi ya mbeleni kwani mpaka sasa wameshafanikiwa kuwaongezea wachezaji kadhaa mikataba.

Kocha wa klabu ya Arsenal ameonesha kufurahishwa na beki huyo wa kimataifa wa Uingereza, Huku akisema beki huyo ni kiongozi na na anapenda kushinda, lakini pia amekua kiongozi wa mfano klabuni hapo na wamefurahishwa kuendelea kua nae zaidi klabuni hapo.ben whiteBen White atakua klabuni hapo mpaka mwaka 2028 hivo ameongeza miaka minne ya kuendelea kuwatumikia vinara hao wa ligi kuu ya Uingereza, Kwani beki huyo yupo kwenye mpango wa muda mrefu ambao klabu hiyo inao chini ya kocha Mikel Arteta.

Acha ujumbe