Klabu ya Norwich City iliyopanda EPL imetangaza kumsajili mchezaji Billy Gilmour kutoka Chelsea kwa mkopo akitokea Chelsea na atahudumu klabu hii mpya kwa muda wa mwaka mmoja mmoja, yaani 2021/2022.
Billy Gilmour ambaye alijiunga na akademi ya Chelsea mwaka 2017 akitokea Rangers amefanikiwa kucheza mechi 22 za timu ya wakubwa kuanzia mwaka 2019.
Gilmour ana miaka 20 tu lakini uwezo wake ni mkubwa na ndiyo sababu ya Chelsea kumtoa kwa mkopo kwenda Norwich ili aweze kuboresha kipaji chake na kuendelea kuwa na ubora zaidi kabla ya kurejea Stamford Bridge.
Mchezaji huyu raia wa Scotland, licha ya umri wake mdogo alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Scotland waliocheza michuano ya Euro 2020 kabla ya kuondolewa katika mchezo wa mwisho baada ya kupata Korona.

Kwa upande wa Norwich wao wanaamini kuwa Billy atakuwa na mchango mkubwa kwao kutokana na ukweli kuwa wameuza baadhi ya viungo tegemezi wa kikosi chao cha kwanza punde tu baada ya kupanda daraja!
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

