Conte Alisubiri Sana Kuitwa United, Hadi Dakika ya Mwisho

Meneja mpya wa Tottenham Hotspurs, Antonio Conte anatajwa kuwa alisubiri hadi dakika ya mwisho kuona kama Man United wangemtimua Ole Gunnar Solskjaer na kumpa kibarua klabuni hapo.

Tottenham walimtangaza Conte kama meneja wao mpya mwanzoni mwa mwezi Novemba, akipewa mkataba wa miezi 18 klabuni hapo.

Kabla ya kukubali dili hilo, kocha huyu alikuwa anahusishwa na kuirithi nafasi ya Ole Gunnar ikiwa Manchester United wangemtimua meneja wao wa sasa, akiungana na Zinedine Zidane kama wanaopewa nafasi zaidi.

Antonio Conte
Aliamua kuchukua kibarua cha umeneja Tottenham

Lakini Zinedine Zidane tayari alishaweka wazi kuwa hatua inayofuata kwake ni kufundisha timu ya taifa, hii ilimpa nafasi na matumaini zaidi meneja wa sasa wa Spurs.

Hata hivyo, Conte aliamua kumbadili Nuno Espirito Santo pale Spurs, na kwa mujibu wa mwandishi Roberto Gotta, Conte amesubiri sana kwenda United, hadi dakika ya mwisho.

Kwa mujibu wa mwandishi huyu, bosi huyu alifanya maamuzi sahihi kuchagua kwenda Spurs.


 

MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.