Crescentus Magori Aipongeza Simba SC, Asisitiza Mechi Zote Ziwe Zina Ushindani

Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC, Crescentus Magori, ampongeza kikosi chake kwa ubora wa michezo yao na kuhimiza ligi ya Tanzania kuendelea kuwa na ushindani wa kweli.

Crescentus Magori Aipongeza Simba SC, Asisitiza Mechi Zote Ziwe Zina UshindaniAkizungumza baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Pamba Jiji, Magori alisema.“Ligi nzuri ni ile ambayo kuna timu zake zinafungwa, kusare na kushinda na tukiacha mpira uchezwe bila maigizo ndio tutapata ubora wa ligi yetu, ndio maana mechi zetu zote za Simba SC ni bora hakuna maigizo, mechi za Simba SC ndio zinavutia.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Aliongeza kuwa: “Pamba Jiji walikuwa vizuri, walikuwa bora na tunategemea mechi zote acheze hivi ndio tutaona ubora wa ligi yetu, kuna timu hapa utashangaa zinafungwa goli nne hadi tano.”

Kauli hizi zinaonyesha wazi msimamo wa bodi ya Simba SC kuhakikisha kila mechi inakuwa na ushindani wa hali ya juu, huku ikionyesha kuwa mashabiki wanastahili kuona michezo yenye mvuto na ushindani wa kweli.

Crescentus Magori Aipongeza Simba SC, Asisitiza Mechi Zote Ziwe Zina UshindaniMagori ameendelea kusisitiza umuhimu wa timu zote kucheza kwa uwazi na bila maigizo ili kuongeza umaarufu na kiwango cha ligi ya Tanzania, ikiwemo kuimarisha michuano ya ligi kuu ya NBC.

Kauli yake pia ni ishara kwa timu nyingine nchini kuwa ushindani wa kweli ndio unachochea maendeleo ya soka na kuvutia mashabiki wengi zaidi kwenye viwanja.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.