Kikosi cha Simba SC kimerejea Dar es Salaam kikitokea Mwanza, ambako kilicheza dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mchezo huo ulipigwa katika dimba la Uwanja wa CCM Kirumba, ambapo timu zote zilionesha ushindani mkubwa na kugawana alama moja kila upande baada ya dakika 90 kukamilika.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Baada ya matokeo hayo, Simba sasa inaelekeza nguvu zake katika mchezo mwingine wa ligi dhidi ya TRA United, utakaochezwa Machi 22. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na umuhimu wa alama tatu kwa kila timu.
Timu hizo zitakutana katika uwanja wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, kuanzia majira ya saa 1:00 usiku, huku mashabiki wakitarajiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo.
Huo utakuwa mchezo wa 14 kwa Simba SC katika msimu huu wa ligi, wakati TRA United wao utakuwa ni mchezo wa 16, hali inayoongeza presha kwa pande zote mbili kutafuta ushindi.

