Dube Aendelea Alipoishia.

Katika mwendelezo wa Ligi kuu ya NBC hapo jana mshambuliaji wa Azam FC Prince Dube ameendelea alipoishia baada ya kufunga bao kwa mara ya pili mfululizo kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu.

 

Dube Aendelea Alipoishia.

Dube ameendelea hivyo baada ya kuipatia timu yake pointi tatu muhimu kwenye mechi iliyopita dhidi ya Simba na jana pia amefanya hivyo Bao hilo lilifungwa katika dakika ya 56 huku Yahya Zayd akitoa pasi ya bao.

Mchezaji wa Ihefu Juma Nyoso aliigharimu timu baada ya kupewa adhabu ya kadi nyekundu baada ya kucheza rafu mbaya ambayo ilifanya mwamuzi amuadhibu na kufanya timu yake kucheza wakiwa pungufu, kitu ambacho kikapelea Dube kuwaadhibu na  huenda labda angekuwepo wangeambulia hata sare lakini wapi.

Kutokana na ushindi huo wa jana Azam FC wamesogea hadi nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Ligi kuu baada ya kufikisha pointi 17 ambazo ni sawa na Simba japokuwa Wanalambalamba wao wanazidi mchezo mmoja.

Dube Aendelea Alipoishia.

Kwa upande wa Ihefu wao kazi bado ni ngumu baada ya kuwa nafasi ya 14 kwenye msimamo huku ikiwa ni nafasi mbili tu za mwisho amebakiza kushuka mkiani kwani yeye na ambaye yupo nafasi ya mwisho wapo sawa kinachowatofautisha ni mabao ya kufunga na kufungwa.

Baada ya mchezo huo, Dube na wachezaji wenzake watasafiri hadi Morogoro kukipiga dhidi ya Mtibwa Sugar, wakati Ihefu nao watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Simba siku ya tarehe 12 mwezi huu.

Acha ujumbe