Mshambuliaji wa zamani wa klabu za Manchester United na Manchester City Carlos Tevez amepewa mikoba ya kuinoa klabu ya nchini Argentine Rosario Central ambayo inashiriki ligi kuu nchini humo.

Carlos Tevez mchezaji aliyeweka rekodi ya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani, akiwazidi wachezaji bora duniani pindi aliposajiriwa na klabu ya China Shanghai Shenhua mwaka 2016, ambapo alikuwa akivuna kiasi cha $41 million kwa mwaka.

Carlos Tevez

Carlos Tevez alianza maisha yake ya soka kwenye klabu ya Boca Junior na kumalizia Boca Junior, pia amechezea vilabu mbalimbali barani Ulaya na Asia vikiwemo West Ham, Manchester United, Manchester City, Juventus na Shanghai Shenhua.

Carlos Tevez kwa mara ya kwanza anabeba jukumu zito la kuingoza klabu ya Rosario Central kwenye ligi kuu ya Argentine akiwa kama kocha mkuu, huku akiwa amepewa mkataba wa mwaka mmoja kama majaribio.

Je Tevez atawezakurudisha makali yake ya uwanjani akirudishwa kwa njia nyingine ya kuwafunza wengine?


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa