Raisi wa klabu ya Paris Saint Germain Nasser Al-Khelaifi amethibitisha kuwa klabu yake bado haijamfikiria Zinedine Zidane kuinoa klabu hiyo kwa sasa badala yake mikoba inaweza kuwa ya Christophe Galtier.

Awali kulikuwa na tetesi kuwa Zinedine Zidane ndie kocha aliyekuwa anapigiwa chapuo kuweza kuinoa klabu hiyo, huku ikisemekana kuwa bodi ya PSG yote ilikuwa inaunga mkono azamio hilo, kabla ya Christophe Galtier kuingia kwenye kinyanganyiro cha kuchukua mikoba ya Mauricio Pochettino.

Zinedine Zidane

“Tumefanya uchaguzi mwingine kuliko Zinedine Zidane. Tumemchagua kocha ambaye atakuwa bora kwetu kwa ajiri ya kutuweka sehemu tunayostahili.

“Mashabiki watakuwa wamevunjika moyo kumchagua Galtier dhidi ya zidane?, ndoto yetu ni moja, ni uhalisia, kuwa na ndoto kubwa ni kitu kizuri lakini leo, inatupasawa kuwa na uhalisia ukiachana na vyote, hatutaki tena kuwa na muonekana wa ng’ari ng’ari sasa ni mwisho wa mmeto meto tunataka uhalisia.” Alisema Nasser Al-Khelaifi

Pia alisisitiza kuwa klabu ya PSG haikuwai kufanya mazungumzo na Zinedine Zidane kwa ajiri ya kuinioa klabu hiyo.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa