Mnamo tarehe 24 mwezi February mwaka 1977 katika jiji la Michigan nchini Marekani alizaliwa Floyd Joy Mayweather bingwa wa dunia wa mkanda wa uzito wa kati na mwanamichezo Tajiri zaidi duniani. Kwenye historia yake ana mataji ya Dunia 15 ambayo amepambana kama mwana masumbwi wa kimataifa akiwa kapambana kuanzia mwaka 1996-2007,2019-2010, 2011-2015 na kurudi na mpambano ulipoteka hisia za watu wengi sana mwaka 2017.

Mayweather anatajwa kama mwanamasumbwi bora wa Muongo wa 2010, kwa mwaka 2016 Chombo cha habari za ESPN kilimtangaza Mayweather kama mwana masumbwi Bora wa kipindi ya Miaka ya 2010. na kua bondia bora wa uzito wa kati kwa kipindi chote.
Mara zote anatambulika kama mwana masumbwi anaejiami zaidi kwenye historia, akitajwa kwa ushindi mfululizo wa mapambano zaidi ya 26 akiwa na ubingwa wa dunia kwa KO 10, ushindi wa mapambano 23, KO 9 katika shindano la Linear, Ushindi mara 24 na KO 7 alipokutana na mabingwa wenzie wa Dunia, Ushindi mara 12, KO 3 katika mashindano aliyokutana na mabingwa wenzie wa Linear na Ushindi mara nne na KO moja kwa mashindano ya kawaida ya kimataifa.

Mayweather ni moja ya watu wenye ushawishi wa kuwaangalia kwa malipo wa muda wote na katika michezo yote. Ameripotiwa na Jarida la Forbes kua ndie mwanamichezo aliyelipwa zaidimwaka 2012 na 2013 na kuandikwa tena 2014 na 2015 ikimtaja kua ndie mwanamichezo anaelipwa zaidi Duniani.
Huyo ndie Mayweather aliyebadirisha ndoto ya mtaa kua mfereji wa Fedha kwa kukazia kwenye ndoto ya kuwakalisha watu kwenye ulingo.


Issa
Floyd mayweather ni moto