Hizi hapa hesabu za Mgunda Dabi ya Kariakoo

Kocha Mkuu wa Simba JUMA Ramadhan Mgunda, ameweka wazi kuwa kwa sasa akili zake ni kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambao utapigwa wiki.

Mgunda anafanya kazi kwa ushirikiano na Seleman Matola wote wakiwa ni wazawa wamefanikiwa kukiongoza kikosi hicho kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Oktoba 23,2022 Uwanja wa Mkapa mchezo wa Kariakoo Dabi unatarajiwa kuchezwa ambapo kila timu inahitaji pointi tatu muhimu.

Mgunda ameweka wazi kuwa walikuwa wanapiga hesabu kwenye mechi zao za kimataifa jambo lililowafanya wafanye vizuri baada ya kazi kuisha sasa wanarejea kwenye ligi.

“Kwenye kila mchezo ambao unatukabili ni muhimu kufanya maandalizi mazuri na ninajua kwamba wapinzani wangu, (Yanga) wapo imara hivyo nasi tunajipanga kupata matokeo.

“Kikubwa ni utayari na wachezaji wanajua kwamba kuna haki na wajibu, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwenye mechi zetu zote ambazo tunacheza,”.

Mgunda amebainisha kuwa anawatambua wapinzani wake Yanga kwa kuwa amekutana nao mara nyingi kabla hajawa ndani ya Simba.

Timu zote ndani ya ligi baada ya kucheza mechi tano zimekusanya pointi13 na hakuna timu ambayo imepoteza mchezo wake msimu wa 2022/23.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.