Klabu ya Chelsea ipo mbioni kupata kiasi kikubwa cha fedha kupitia Jeremie Boga iwapo kiungo huyu nyota wa kikosi cha Sassuolo atauzwa.
Nyota huyo wa Sassuolo anahusishwa na dili la kusajiliwa na timu ya Ufaransa ‘Rennes’ ambayo imeweka mezani ofa ya pauni 17m ili kunasa saini ya nyota huyo.
Mkurugenzi wa Chelsea, Marina Granovaskaia alifanikiwa kuweka kipengele kinachowawezesha Chelsea kupata 15% ya ada yoyote ambayo mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea atasajiliwa na timu nyingine.
Jeremie Boga (23), aliyekuwa na mafanikio makibwa katika misimu miwili iliyopita, anawaniwa wa vilabu vya Napoli, Roma na Atalanta lakini Rennes ndiyo wapo karibu zaidi kupata saini ya nyota huyo.
Nyota huyo ambaye ni zao la kituo cha kukuzia vipaji cha Chelsea, amejipatia uzoefu mkubwa mara baada ya Chelsea kumpeleka kwa mkopo katika vilabu mbali mbali vya ligi za La Liga, Championship na Ligue 1 kabla hajaamua kuihama mazima klabu hiyo ya London mwaka 2018.
Kwa upande wa Boga mwenyewe, yupo tayari kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine nje ya Sassuolo na Rennes ndiyo panapoelekea kuwa kituo chake kinachofuata.
Kocha wa Rennes, Julien Stephan ameweka wazi kuwa anavutiwa na mchezaji huyo wa Sassuolo na yupo tayari kumsajili.
“(Jeremie Boga) ana uwezo mkubwa wa kukaa katika nafasi, kutengeneza na kumalizia mashambulizi. Ninamfahamu vema kwa kuwa alishaichezea timu hii kwa mkopo misimu michache iliyopita. Mimi na yeye tunafahamiana, japo kipindi hicho nilikua nafundisha kikosi cha pili cha timu hii.”
Katika hatua nyingine, kaka wa Boga, ambaye pia ni wakala wake, amesema kuwa Boga anawaniwa na timu nyingi za Seria A na EPL lakini maamuzi juu ya wapi atakwenda ni juu yake mwenyewe.
Kwa upande wa Chelsea wenyewe, watapata 15% ya ada ya usajili itakayotolewa na klabu yoyote itakayomsajili Boga.
SHINDA NA HI LO
Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.


Johnmary joel
Pongezi nyingi kwake#meridianbett
Rehema
Hongera
magdalena
bonge moja la dili likikamilika chelsea hawatakuwa na njaa tena
Dorophina
Bonge la dili kwa Chelsea wakifanikiwa kumuuza mchezaji wao
aisha
Iyo ndo faida team kukuza vipaji baadae km ivi inaleta kweny team pale anapouzw
Mwajumah
Ilo ni dili kubwa kwa chelsea wakifanikisha hakika watatusua sana#Meridianbettz
Rehema Dickson
Hongera sana kwake
Shani
Dili limekaa powaaa!
Adelta
Anastahili kupewa pongezi
@meridianbettz
Ernest
Hapa faida inaingia kote Chelsea na kwa Sassuolo
Caroline
Mambo ya pesa ayo
Nasra
Safii
Lydia Emmanuel Magoti
Bonge ladiri Chelsea pesa Zina wanukia
Hidaya
Pesa ndio mpango mzima
felister
bonge moja la dili
Mwanahamisi
Hongera sana kwake
Hidaya
Kwenye pesa hakuna kinachoshindikana
Furahav
Safi
Tatu
Safi sana Chelsea bonge la dili
Khadija
Dili limekaa poa#meridianbettz
Povel
Deal done
Frank P
Wenzetu hapa wanachezaga sana hapa wanajua kupiga hela kupitia mikataba
Saupha mohamed
Hongera sana
Sauda
Hongera sana kijana
Fatuma kasomo
Dili limetiki
Agness
Hongera zake
Amiri Kayera
Ndo faida ya kulea vipaji saf
Neema
Bongee la dilii hilo
Theonestina
Hongera yake
Rose kapinga
Kibiashara zaidi pesa mbele mengine baadae!!!
Genia Sikaluzwe
Hongera
Sabrina
Big up broh
Shafii
Chelsea wamekua wajanja Sana kwenye vipengele vya wachezaji kwenye mikataba yao hili lilionekana pia kwenye kipengele cha Edin hazard.
Ester jackson
Hapana chezea hela na Chelsea wako vizuri kwa ujumla na hela mana hapo ni dili kubwa sana la kuwaingizia hela Chelsea pia tukumbuke kuwa pia kunamchezaji ambaye anaingizia timu hiyo hazard ambaye anaichezea real Madrid
JULIANA
Safi
Issa
The blues wanafaidika kwa vipaji vyao
Hope mwaikuka
💪
Sadick
Mkurugenzi Marina Granovaskaia amekuwa na mbinu wa kuweka vipengele vinavyoinufaisha Chelsea baadaye#meridianbettz
Gabriel
Pesa ndio mpango mzima
warda
Unaambiwa pesa inaongea