Lamine Yamal Apata Hamasa Kutoka kwa LeBron James, Neymar Kabla ya Kuwakabili Atletico

Winga chipukizi wa FC Barcelona, Lamine Yamal, amesema anapata hamasa kutoka kwa nyota wa mpira wa kikapu LeBron James pamoja na staa wa Brazil Neymar Jr kuelekea mchezo wa marudiano wa robo fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Atletico Madrid.

Lamine Yamal Apata Hamasa Kutoka kwa LeBron James, Neymar Kabla ya Kuwakabili AtleticoBarcelona wanakabiliwa na kibarua kigumu baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 2-0 nyumbani, lakini wanatarajia kufanya comeback katika dimba la Metropolitano ili kufuzu hatua ya nusu fainali kwa msimu wa pili mfululizo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Yamal alieleza kuwa alibadilisha picha yake ya wasifu kwenye Instagram na kuweka picha ya LeBron James alipobeba kombe la NBA mwaka 2016, aliposaidia Cleveland Cavaliers kufanya comeback ya kihistoria dhidi ya Golden State Warriors. “Ni mmoja wa watu wanaonipa hamasa kwa mchezo wa kesho, ndiyo maana niliweka picha yake. Nitafikiria alichokifanya na natumaini itanisaidia pia,” alisema Yamal.

Lamine Yamal Apata Hamasa Kutoka kwa LeBron James, Neymar Kabla ya Kuwakabili AtleticoAidha, Yamal alimtaja Neymar kama chanzo kingine kikubwa cha msukumo, akirejea comeback maarufu ya Barcelona mwaka 2017 dhidi ya Paris Saint-Germain, ambapo waligeuza kipigo cha 4-0 kuwa ushindi wa 6-1. Nimeutazama ule mchezo mara nyingi na hata niliuona moja kwa moja. Neymar ni idol wangu, amenipa mengi sana kwenye mpira,” aliongeza.

Katika mchezo wa kwanza, Yamal alikumbana na ulinzi mkali kutoka kwa Atletico, akifuatwa na mabeki wawili au watatu kila alipokuwa na mpira. Kocha wa Barcelona, Hansi Flick, alimtaka kijana huyo kuendelea kutumia ubora wake kwenye hali za mmoja kwa mmoja.

Lamine Yamal Apata Hamasa Kutoka kwa LeBron James, Neymar Kabla ya Kuwakabili AtleticoKwa upande wake, Yamal amesema ana matumaini ya kupata uhuru zaidi katika mchezo wa marudiano. “Ninajisikia vizuri na ninasubiri kwa hamu mchezo wa kesho. Natumaini nitaweza kuleta tofauti. Tutaona kama kocha wao atanipa nafasi ya kuwa mmoja kwa mmoja na mchezaji,” alihitimisha.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.