Nasreddine Nabi Kocha Mkuu wa Yanga SC, ameweka wazi kuwa anafurahi kuona winga wake, Jesus Moloko amerejea kikosini mapema baada ya kupata majeraha walipocheza dhidi ya Coastal union, huku akiweka wazi kuwa ana matumaini makubwa ya kumtumia staa huyo katika mchezo dhidi ya Azam FC.

Mchezaji huyo tayari ameanza mazoezi ya pamoja, na kikosi cha timu hiyo mara baada ya kupata majeraha katika mchezo wao waliopata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kocha Nabi Anamtaka Moloko Dhidi ya Azam FC
Mshambualiaji wa Yanga SC-Moloko Jesus

Baada ya ushindi kwenye michezo yao miwili ya ugenini dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union, Yanga SC sasa inajiandaa na mchezo wao wa mzunguko wa tatu dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Septemba 6, mwaka huu.

Kocha Nabi alisema: “Ni jambo zuri kuona Moloko ameanza tena mazoezi baada ya kuwepo tishio la kumkosa katika mchezo wetu dhidi ya Azam FC, kutokana na majeraha ambayo aliyapata tulipocheza dhidi ya Coastal Union, Arusha.

Kocha Nabi Anamtaka Moloko Dhidi ya Azam FC

“Ni wazi amekuwa kwenye kiwango bora sana tangu kuanza kwa msimu huu na kuelekea katika mchezo wetu mgumu ujao, dhidi ya Azam ni matarajio yetu kuwa atakuwa amerejea katika utimamu wa asilimia 100.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa