Trevoh Chalobah beki kinda wa klabu ya Chelsea anatarajiwa kubakia ndani ya klabu hiyo baada ya mwanzo kutaka kutolewa kwa mkopo kuelekea mbili kati Ac Milan na RB Leipzig.

Mchezaji huyo aliekua anatarajiwa kutolewa kwa mkopo kupisha usajili mpya wa beki mpya aliesajiliwa klabuni hapo kutoka klabu ya Leicester city Wesley Fofana.

trevoh chalobah

Chelsea inasemekana ndio wamezuia Trevoh Chalobah kutolewa kwa baada ya kusitisha mazungumzo na vilabu vyote vilivyohitaji huduma ya mchezaji huyo kwa mkopo ikiwemo Ac Milan na RB Leipzig.

Hii imekuja baada ya mazungumzo ya ndani baina ya kocha wa timu hiyo Thomas Tuchel na bosi wa timu hiyo Todd Boehly na kuafikiana mchezahi huyo asalie klabuni hapo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa