Ajax na Man United wamefikia makubaliano juu ya mchezaji Antony raia wa Brazil ambaye alikua anawindwa na Man United akitokea Ajax sasa ni rasmi nyota huyo ataelekea nchini Uingereza kujiunga na mashetani hao wekundu baada ya dau lao kukubaliwa la euro milioni 100 na miamba hiyo ya soka nchini Uholanzi.

 

Klabu ya Man united imekua ikimuwinda mchezaji huyo tishio wa klabu ya Ajax kwa mudan miezi miwili na ofa kadhaa zikikataliwa na miamba hiyo ya soka nchini uholanzi lakini kufikia taarifa zimetoka klabu imekubali dau hilo na kumuachia nyota huyo fundi wa mpira.

ajax

Antony anakua mchezaji wa tano kusajiliwa ndani ya klabu hiyo majira haya ya joto, Pia anakua mchezaji wa pili kusajiliwa akitokea klabu ya Ajax baada ya United kukamilisha usajili wa beki Lisandro Martinez.

United wamepata  kukamilisha dili la mchezaji baada ya mchezaji mwenyewe kulazimisha kuondoka klabuni hapo na uelekeo wake akawa ni kwa mashetani hao wekundu baada ya kumalizana nae kwenye maslahi binafsi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa