UONGOZI na benchi la ufundi la Simba SC kupitia kwa kocha wao msaidizi, Selemani Matola, umeweka wazi kuwa unaamini michezo miwili ya kimataifa dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana na Al Hilal ya Sudan watakayocheza nchini Sudan, ni kipimo sahihi kwao na itawasaidia kuwa tayari kwa ajili ya mipango yao ya kufanya makubwa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Waghana Waipa Jeuri Simba SC
Kocha Msaidizi wa Simba SC-Seleman Matola

Sehemu ya kikosi cha Simba SC juzi Alhamis kiliondoka nchini kwenda Sudan kwa ajili ya michuano midogo ambapo wanatarajia kucheza michezo miwili dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana utakaopigwa Leo Agosti 28, kabla ya kuvaana na Al Hilal Agosti 31, mwaka huu.

Waghana Waipa Jeuri Simba SC
Simba SC katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wataanzia hatua ya awali ambapo wamepangwa kucheza dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi wakianzia ugenini Septemba 9, mwaka huu na kurudiana Septemba 16, mwaka huu.

Matola alisema: “Tunatarajia kuanza na Nyasa Big Bullets ya Malawi katika hatua ya awali ya mashindano Ligi ya Mabingwa Afrika, tumewafuatilia na kujua tunakwenda kucheza na timu ngumu kulinganisha na wengi wanavyofikiria.

“Hivyo kupata michezo hii miwili ya kimataifa ya kirafiki imekuwa jambo muhimu kwetu kwa kuwa tunakwenda kucheza dhidi ya mabingwa wenzetu, tunaamini kuwa baada ya kutoka katika mashindano haya tutakuwa na utayari wa kufanya vizuri katika mashindano haya na kufikia malengo tuliyojiwekea.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa