Nyota wa zamani wa Barcelona, Neymar Jr anasema kuwa a nafurahia ukweli kuwa yupo kwenye fomu nzuri tangia alipojiunga na klabu ya Paris Saint Germain – PSG.
Inakumbukwa alitimba PSG akitokea Barcelona kwa rekodi ya dunia ya Euro milioni 222. Neymar ameshinda mataji 9, amefunga magoli 74 katika mechi 84 za michuano yote.
Staa huyu ambaye amekuwa akihusishwa na kurejea LaLiga, tayari ameshainua Ligue 1, Coupe de France, Coupe de la Ligue na Trophee des Champions wakati wakiwa wanalitupia macho taji la Ligi ya Mabingwa sasa.

“Miaka hii mitatu imekuja na mafundisho mengi. Nimeishi vipindi vya furaha na baadhi ya vipindi vigumu. Hasa niliposhindwa kucheza kwa sababu ya majeraha.”
“Kwa msaada wa wachezaji wenzangu, niliweza kushinda na kuzingatia kwenye kile kilichokuwa muhimu kwa kila mtu.” -Neymar
Neymar anasema anaishi nyakati bora zaidi akiwa Paris, wakati wakiwa wanajiandaa na kibarua walichonacho kwenye Ligi ya Mabingwa.
Tiketi yako ya kwanza kamwe haiwezi kupoteza ukiwa na Meridianbet. Unarudishiwa 100% ya Tiketi yako ya kwanza.


Mwanahamisi
Asante kwa taarifa
Ester jackson
Ni habari njema sana kwa sisi mashabiki wake kutujuza kuwa yuko vizuri tokea ahamie PSG
Mwajumah
Habari njema
magdalena
pongezi zake kwa kupata nafasi ya kukaa sehemu ambayo anajiona yupo vizuri
warda
Namkubali sana Neymar jr#Meridianbettz
Caroline
Usiondoke P.S.G. neymar.ni timu kubwa iyo
Zeiyana
Neymar kwa ustaa wake wote alio kua nao lakini PSG hanonekani zaidi ya mbappe tu yota yake hime kufa
Antony Luseno
Tatizo ni ujana mwingi ila mpira anaujua mno
Dorophina
Neymar talent player
Nasra
Neymar kiungo bora
Sauda
Hongera Neymar kwa rekodi nzuri
felister
tatizo la Neymar ubishoo mwingi
Adelta
Neymar Yuko vizuri sana
#meridianbettz
Njiku
Kweli kabisa maana anacheza kwa uhuru wa hali ya juu ana combination nzuri na wachezaji wenzake ipo poa sana
aisha
Neymar ni mchezaji mzuri
Tatu
Neymar anajua mpira tatizo maringo
Fatina mfingi
Neyrmar yupo vizur
Zuhura omary kindamba
Ney mar yupo vizuri
Sadick
Nilitamani kuona Neymar akibaki Barcelona kuendeleza utatu maridadi kati yake na Messi na Suarez ambao uliwapa mafaniko makubwa#meridianbettz
Latifa juma mohamed
Gud congr neymer
Khadija
Habari njema#meridianbettz
Salma ngende
Habari nzuri
Tahiya
Neryma namkubali yuko vizur na timu pia imekpokea vyema
Neema juma
Neymar mchezaji makini mno
Shafii
Neymar tokea atue PSG sijaona bado mchango wake kwenye timu ya psg Kama mchezaji mkubwa.
Rehema
Hii ni habari mzuri
Issa
Neymar anatumia jina tu lakini kwa soka halina kiwango sana
Saupha mohamed
Neymar saiv ana maajabu
Frank
Kwa idadi hii ya mabao angekuwa epl or la liga mchezaji bora wa dunia angelikuwa yeye
Gabriel
Habar njema
Fatuma kasomo
Nihabari nzuri
Devotha
Namkubali sana Neymer
farida ahmadi
Hakika neymar Yuko vizuri Sana
Amiri Kayera
Neymar akiach utoto ni mchezaj mzur sana
Samiah
Neymar yupo vzr
Hope mwaikuka
Neymar nae bishoo sana
Ernest
Watu wengi tumekuwa tukitaka kuona Neymar anapata mafanikio zaidi ambayo alitamani kupata wakati akiwa Barca, Binafsi natamani kumuona akiendelea kukipiga PSG
Lydia Emmanuel Magoti
Nikweri unacho kiungea upo sahii lakini uwache ubishoo ukiwa ndani yauwanja jembe
Furahav
Bado yuko vizuri.
Sabrina
Ney mar talent prayer
David Pere
Acheze mpira Sasa