Real Madrid tayari walipoteza dhidi ya Man City wa kichapo cha 2-1 kwenye mechi iliyopita kabla ya “lockdown” , na sasa wanaamini huu ni wakati muafaka kuelekea kulipa kisasi.
Mechi ya Ligi ya Mabingwa kati ya mabingwa hawa wa LaLiga, dhidi Manchester City walioshindwa kutetea ubingwa wao EPL, itachezwa bila mashabiki.
Kwa mujibu wa Casemiro kucheza katika dimba ambalo halina mashabiki itakuwa ni nafuu katika mpango wao wa kulipa kisasi na kuondoa kuondoa hasara ya kupoteza mechi iliyopita.
Ni mechi ngumu zaidi kwa Real Madrid, wanaosafiri kwenda dimbani Etihad kwenye mechi ya mzunguko pili wa mtoano wa timu 16 kuelekea robo fainali. Real wanataka kubadili matokeo ya 2-1 waliyoyapata kabla ya Corona.
Bila shaka, vijana wa Guardiola wanaenda kuingia dimbani wakiwa na hasira na majuto ya kushindwa kutetea ubingwa wa EPL, na wanaichukulia hii kama nafasi muhimu ya kuendelea kuwika Ulaya. Ni wazi Real Madrid wana kibarua kizito tarehe 8, Agosti.
Wakati Real Madrid wakiwa na mlima wa kupanda Casemiro anaamini kuwa vijana wa Zidane watafaidika na kutokuwepo mashabiki uwanjani.
“Bila mashabiki mchezo ni mwingine kabisa. Utakuwa mchezo mzuri sana na mgumu kwa pande zote, lakini sisi ni Real Madrid na tunafahamu tunayo nafasi ya kusonga mbele.”
“Hawatakuwa na mashabiki hiyo itakuwa nafuu kwetu kiasi. Wachezaji ni wale wale, mwalimu ni yule yule na wote tunaelewa kiwango cha ugumu kitakuwa vile vile kwa kuwa ni timu kubwa.”
Tiketi yako ya kwanza kamwe haiwezi kupoteza ukiwa na Meridianbet. Unarudishiwa 100% ya Tiketi yako ya kwanza.


Caroline
Tuone Kama watalipa icho kiasi
Caroline
Tuone Kama watalipa icho kisasi
Adelta
Good news
Ester jackson
Kweli kabisa itakuwa mchezo mgumu sana huo mana ukizingatia wote wako vizuri hasaivi na wanaendekea vizuri ukiangalia upande wa zidane yuko vizuri hasaivi tumeona dakika za mwisho kabisa anavyo onyesha uwezo wake kupanda mpaka akampita mpizani wake kutoka Barcelona kwa kumzidi point nyingi hivyo anaweza kubadilisha matokeo ya kufugwa 2-1
Mwanahamisi
Gud news
Mwajumah
Gud .news
magdalena
madrid kwa city wajipange sana maana city ni moto wa kuotea mbali wakiamua
Dorophina
Sidhani kama madrid wataweza kulipa hiko kisasi maana man city wapo miamba tupu
warda
Nawakubali sana Madrid#Meridianbettz
Sauda
Madrid wanaweza
Zeiyana
Mtanange hutakua si wahaina yake
Nasra
Gud news
felister
itakua mechi ngumu sana
Njiku
Mechi ngumu sana acha tuone kama watalipa kisasi au watachapwa tena
aisha
Madrid wanaweza
Tatu
Mpira bila mashabiki sijui itakuwaje
Fatina mfingi
Mpira bila mashabiki unapooza sanaa
Zuhura omary kindamba
Habali njema kabisa
Sadick
Real Madrid inaamini kombe ni lake, kana kwamba haina mpinzani. Mchezo utakuwa mgumu sana#meridianbettz
Latifa juma mohamed
Real Madrid nawakubali sana
Salma ngende
Itakuwa poa
Tahiya
Hakika itakuwa gemu nzur sana
Neema juma
Tunasubiria kuona km wataweza kulipa kisasi
Shafii
Bila mashabiki itakua haileti molari ya mpira maana inasadikika mshabiki ni mchezaji wa kumi na mbili uwanjani.
Rehema
Iko poa
Issa
Madrid ni ndoto kuitoa city city ndio kombe wanalolitegemea
Saupha mohamed
Good news
Frank
Ngoja tuone kama kweli uefa inauzoefu
Fatuma kasomo
Gud news
Povel
Don’t miss
Devotha
Yetu macho kutazama dk 90 Kama kweli atalipa kisasi au atachapwa tena
farida ahmadi
Sio mbaya kikubwa kinachotakiwa ni kufanya vizuri
Amiri Kayera
Mechi itakua babkubwa
Samiah
Duuh itakuwa balaaa
Hope mwaikuka
Habar nzur hii
Ernest
Hii ni mechi ya kukata na shoka na yenye mvuto mkubwa sana kwenye UEFA
Lydia Emmanuel Magoti
Duu ilikuwaje bila mashabiki
Furahav
Ngoja tusubili tuone itakuaje.
Sabrina
Raha ya mpira mashabik
David Pere
Lazima walipze kisasi