“Nimeota vya Kutosha! Imetimia!” - Ole

Ilikuwa kama stori lakini imegeuka na kuwa historia sasa. Man United wamemkabidhi mikoba ya kudumu kocha wao aliyekuwa anaiongoza klabu hiyo kwa muda, Ole Gunnar Solskjaer baada ya kipindi kirefu cha uangalizi wa klabu hiyo. Wameridhika na uwezo wake katika siku za mwanzo tu hizi na kuamua kumkabidhi mikoba ya kudumu.

Wamempa mkataba utakaoisha 2022 ikiwa ni baada ya kukubaliana na uwezo wake aliouonesha kipindi alichokuwa na kikosi cha matajiri hao. Hakuna aliyepingana na uteuzi huo uliofanywa na klabu hiyo kutokana na matokeo aliyoyaonesha kwa kipindi hicho kifupi alipopewa klabu.

Solskjaer amefaidika na ushindi wa mechi 14 kati ya 19 alizocheza baada ya kushika mikoba ya mtangulizi wake, Jose Mourinho aliyeondoshwa baada ya kushindwa kufanya kile ambacho klabu hiyo ilikuwa ikikitazamia. Baada ya kocha huyo kupewa mikoba hiyo aliweza kurejesha hali upya na kuonesha mafanikio yaliyokubalika na wengi.

Ni dhahiri kwamba United waliweka wazi kwamba wangetangaza mtu ambaye angeishikilia nafasi hiyo kabla ya msimu huu kuisha; lakini baada ya fununu juu ya kupata muwakilishi wa kudumu wa kikosi hicho kuzidi kushika kasi na msukumo wa baadhi ya wakongwe kwamba anastahili kupewa nafasi hiyo; wameamua kufikia makubaliano hayo mapema na kutangaza.

United wanategemea kucheza mchezo wa ligi siku ya Jumamosi na Watford na ni kwa wakati huo ambapo kocha huyo atakaribishwa vizuri na mashabiki wa klabu hiyo kwa furaha zote ndani ya viwanja vya Mashetani Wekundu. Atapokea ukaribisho wa mara ya pili ikiwa ule wa awali haukuwa rasmi sana kwake.

Ole anadai kwamba hiyo ni kazi yake ya muda mrefu ambayo siku zote alikuwa akiitamani na kwa uhalisia uliopo anajiona mwenye bahati sana kupata nafasi ya kuhudumu kwa kipindi kirefu zaidi katika ardhi hiyo ambayo amekulia kisoka na ameweza kuweka historia yake ya pekee ndani ya ardhi hiyo na hapo kwake patabaki kama nyumbani kwake.

Kocha huyo sio kwamba pekee ameweza kupunguza uwiano mkubwa wa alama uliokuwepo kati yao na kinara wa ligi hiyo bali ameweza kwa upande mwingine kuifanya klabu hiyo iweze kufika hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa mara ya pili tangu ilipotokea mwaka 2011.

Ukiweka mbali historia aliyoiweka katika klabu hiyo kwa makubwa aliyoyafanya   miongoni mwa vitu havitasahaulika kwenye maisha yake ya soka kwa siku za usoni ni lile alilofanya mbele ya PSG baada ya kufanikiwa kuwatupa nje ya michuano hiyo kutoka kupoteza mchezo wa awali hadi kushinda mechi hiyo na kufanikiwa kusonga mbele. Jambo hilo haliwezi kusahaulika kwenye maisha yake binafsi na maisha ya kila mmoja anayefuatilia historia ya soka.

Kila la heri Ole!

3 Komentara

    Ukiweka mbali historia aliyoiweka katika klabu hiyo kwa makubwa aliyoyafanya miongoni mwa vitu havitasahaulika kwenye maisha yake ya soka

    Jibu

    Ukiweka mbali istoria aliyo hiweka katika krabu hiyo kwamakubwa aliyo yafanya miongoni mwavitu avito saulika kwenye soka

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.