“Ramos Anastahili Ballon d’Or!” - Figo

Mkongwe wa klabu ya Real Madrid ambaye aliacha historia kubwa kikosini hapo, Luis Figo anaonelea kwamba nyota wa muda mrefu na kiongozi wa wachezaji uwanjani na kikosini hapo, Sergio Ramos anastahili kabisa kuheshimiwa na kupewa tuzo ya Ballon d’Or kutokana na mchango wake aliouonesha kikosini hapo na kwenye timu yake ya taifa.

Ramos [32] ni mchezaji aliyejenga historia kubwa kikosini hapo kwa sasa na kwa kipindi cha nyuma tangu ajiunge na klabu hiyo. Hadi sasa ameisaidia klabu hiyo kunyanyua takriban makombe manne ya klabu bingwa ya dunia; akiwa na wazee wa Los Blancos kitu ambacho kinamfanya azidi kuonekana bora zaidi.

Baadhi ya vitu vinavyoshawishi Ramos aonekane bora zaidi ni kama vile: tangu anunuliwe na klabu ya Real Madrid akiwa kama mchezaji wa Sevilla kipindi hicho miaka ya 2005 Ramos amekuwa mhimili mkubwa ndani ya kikosi hicho jambo ambalo limeonwa na kila shabiki wa soka kwamba nafasi yake ni kubwa mno.

“Ramos Anastahili  Ballon d’Or!” - Figo
Kuwa mlinzi ni changamoto sana kushinda tuzo hiyo kama ilivyo kwa golikipa jambo ambalo kwenye historia ya karibuni tangu kichukuliwe na Cannavaro.

Raia huyo wa Hispania hadi sasa anahusika katika michezo 604 aliyoicheza huku akiwa amefanikiwa kufumania nyavu mara 84 katika nafasi yake ya ulinzi na akiweza kutoa pasi za magoli 39 jambo ambalo ni mageuzi makubwa kwenye soka kwa mtu wa nafasi anayocheza kufanya hivyo.

Hadi wakati huu ameshinda makombe makubwa kumi na hayo yote ni kwa ngazi ya klabu, kombe la dunia pia kombe la Ulaya akiwa na timu yake ya taifa ya Hispania. Hayo ni baadhi tu ya makubwa aliyoyafanya akiwa na klabu yake hiyo na athari zake kushuhudiwa moja kwa moja hata katika ngazi ya taifa.

Msimu uliopita aliiongoza klabu yake hiyo kugombania taji la tatu mfululizo la klabu bingwa Ulaya na ni jambo ambalo alifanikisha akiwa na kikosi hicho hicho cha Madrid. Japo baadaye hawakufanya vizuri kwenye kombe la dunia. Hilo lilionekana kuwa gumu kwa kikosi hicho kutokana na kukosa ushindani.

Figo anasemaje?

Figo yeye anaona kwamba Ramos anastahili na ana kila haki kuipata hiyo tuzo kutokana na msaada mkubwa aliounesha tangu alipoanza maisha yake ya soka la kulipwa hususan kwenye klabu kama hiyo yenye ushindani mkubwa na yenye uwezo kwa kufanya biashara wakati wowote kama wanakuwa wamepata kile walichokihitaji. Hayo ni mambo yanayompa nafasi hiyo kutokana na mchango wake huo.

Kuwa mlinzi ni changamoto sana kushinda tuzo hiyo kama ilivyo kwa golikipa jambo ambalo kwenye historia ya karibuni tangu kichukuliwe na Cannavaro. Japo hili hutegemeana na mwaka husika na ushindani ulipolalia kwa kipindi hicho. Ramos amepitia kila aina ya kipindi akiwa Madrid ikiwemo vipindi vya matunda hata vile vya mpito na ndiyo maana Figo anaona kwamba nyota huyo anastahili zaidi ya hapo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.