Okocha ni moja ya wachezaji bora wa Kiafrika kuwahi kutokea hapa duniani, alifanya mengi sana kwenye mpira, kafunga magoli mazuri na matamu mithili ya mvinyo wa Malkia, anajua kupiga chenga na uwezo wa kukaa na mpira kwa muda mrefu.

Sasa kaacha kucheza soka lakini matukio yake ya mpira bado yanaishi, hapa anaeleza moja ya magoli yake bora zaidi kuwahi kuyafunga ambapo Jurgen Klopp na yeye anaeleza goli hilo ni bora zaidi kwenye Ligi ya Bundersliga, Ilikuwa ni mwaka 1993.

Jay-Jay anauchukua mpira kutoka kwa Uwe Bein huku Oliver Kahn pekee akipiga. Anakataa nafasi ya kupiga shuti kwa kutumia mguu wake wa kushoto, akiuhamishia mpira mguu wake wa kulia kabla ya kumwacha kipa wa Karlsruhe kwenye nyasi akiwa amelala.

Wakati wa kupiga shuti?. Anaruka kushoto, anampiga chenga matata beki mwingine na kugeuka tena upande wake wa kulia, kisha kurudi kushoto kwake. anatulia kidogo, huku Kahn akiwa amepona. Slaven Bilic anakimbilia nje ya mstari ili kushiriki. Lakini anakuwa kachelewa.

Ni bao bora zaidi katika historia ya Bundesliga, kulingana na Jurgen Klopp. Kahn, kipa huyo mzuri wa Ujerumani, anasema bado ana kizunguzungu kutokana na matukio ya mwaka wa 1993. Nyota huyo anaamua kuliita hilo ni goli lake bora katika maisha yake ya mpira.
“Ilichukua muda mrefu zaidi kuliko nilivyotarajia,” anasema.
Wazo la kupiga shuti lilikuja kwanza lakini Kahn alikuwa tayari kakaa kwenye nafasi. “Haikuwa imepangwa unajua ilikuwa ni ‘counter-attack’ na nilipopata mpira nilikuwa na kipa mbele yangu, nikajifanya napiga shuti ili kumtoa lakini hakutaka kuondoka.”
Nilitishia mara ya pili “feint” ambapo golikipa alitishika lakini tayari kulikuwa na walinzi kwenye boksi.
“Nilipokuwa nikijaribu kumchezea chenga, baadhi ya mabeki walirejea. Nilichokuwa nikijaribu kufanya ni kutafuta pengo hilo ili kupiga shuti na, kwa bahati nzuri kwangu, nilifanikiwa kupata hilo,”
alieleza Okocha.
Jay-Jay ni mchezaji wa kiamataifa wa Nigeria aliyefanya makubwa kwenye ulimwengu wa soka, jina lake alilopewa na wazazi wake ni Augustine Azuka Okocha ana watoto wawili Emmanuel na Daniella Okocha.

