Yakiwa ni masaa machache yamesalia kufungwa kwa dirisha kubwa la usajili kocha mkuu wa Leeds United Jesse Marsch amesema kuwa hana matarajio ya kuwa mchezaji wake Daniel James ataondoka klabuni hapo.

Jesse Marsch amerithi mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu wa Leeds Marcelo Bielsa msimu uliopita baada ya Leeds kuwa na hali mbaya kwenye ligi. Hivyo amesema kuwa bado ana uhitaji na mchezaji huyo.
Daniel James alijiunga na klabu hiyo kutoka Manchester United ambapo alipokuwa kule alikuwa hapati dakika nyingi za kucheza lakini pia ushindani wa namba klabuni hapo kitu ambacho kilifanya ajiunge n Leeds United.

Katika kikosi cha Marsch,Daniel James amekuwa akipata nafasi mara mara kitendo ambacho kinamfanya azidi kuimarika siku hadi siku. Leeds katika mechi tano walizocheza wameshinda mechi mbili, sare mbili na wamepoteza mechi moja na wapo katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi.

