UONGOZI wa klabu ya Pan African inayoshiriki ligi ya Championship imemtangaza Iddy Cheche kuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho.

Pan jana jumanne ilitangaza kuvunja benchi lao la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu, Twaha Beimbaya pamoja na Kocha Msaidizi, Hemed Wazir kutokana na matokeo mabaya.

Kocha Cheche aliwahi kukinoa kikosi cha Azam FC kwa mafanikio katika nyakati tofauti akiwa Kocha Msaidizi pia Kaimu Kocha Mkuu.

Cheche tayari ameanza mazoezi na kikosi hicho kuelekea mchezo ujao wa ligi dhidi ya Gwambina utakaopigwa Oktoba 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa