UONGOZI wa Polisi Tanzania umeachana na Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Joslin Sharif kwaa makubaliano ya pande zote mbili kutokana na matokeo mabaya.

Polisi Tanzania ambayo ilianza msimu huu na kocha Joslin katika michezo tisa imefanikiwa kuvuna pointi tano pekee.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro ilieleza kwamba imesitisha mkataba wa kocha kwa makubaliano ya pande zote mbili.

“Klabu ya Polisi Tanzania inapenda kuujulisha umma kuwa imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu, Joslin Sharif kutokana na matokeo yasiyoridhisha tangu kuanza kwa msimu huu wa 2022/23.

“Vile vile Kocha Msaidizi Agustino Damian na Kocha wa makipa Emmanuel Mwansile wao watapangiwa majukumu mengine. Katika kipindi hiki timu itaendelea kuongozwa na kocha wa viungo, John Tamba.

“Aidha uongozi wa timu unaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha timu inafanya vizuri.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa