BAADA ya kutimuliwa kwa kocha Mkuu wa kikosi cha Azam FC, Denis Lavagne, Uongozi wa klabu hiyo umepokea zaidi ya maombi 100 ya makocha wanaotaka nafasi hiyo.

Lavagne raia wa Ufaransa ambaye alijiunga na kikosi cha Azam hivi karibuni alisimamia timu hiyo katika michezo sita na kufanikiwa kushinda mechi tatu na kupoteza tatu.

Akizungumzia mchakato wa kumpata kocha Mkuu, Kaimu Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe alisema tayari wameanza kupokea maombi ya makocha mbalimbali wakihitaji kukinoa kikosi chao.

“Tunamshukuru Mungu kikosi kipo salama tayari kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Simba chini ya Kaimu kocha Mkuu, Kali Ongala.

“Tumepokea CV za makocha mbalimbali ambao ni zaidi ya 100 kutoka ndani na nje ya Tanzania wakihitaji kufanya kazi ya kukinoa kikosi chetu.

“Uongozi unaendelea kuyafanyia kazi na mchakato ukikamilika basi kocha atatangazwa. Hakuna asiyetamani kufanya kazi na kocha kariba ya Nabi lakini tunamheshimu kwani yupo kwenye timu nyingine.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa