Pep Guardiola Amtaka Harry Kane

Klabu ya Manchester City inataka kufanya mpango wa kutenga pauni Milioni 90 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola anataka kufanya hivyo ili kufanikisha mtu sahihi wa kuziba pengo la Sergio Aguero ambaye anasumbuliwa na majeraha.

Kane amekuwa mmoja wa washambuliaji wenye ubora wa juu kwa msimu kadhaa sasa, amekuwa akifunga mabao 20 au zaidi katika michuano yote kwa misimu sita iliyopita na ameshinda Tuzo ya Ufungaji Bora wa Premier League, mara mbili.

Kane amekuwa na nguvu kubwa pia katika timu ya taifa ya England na hata ngazi ya klabu akiwa na uwezo wa kufunga na kutoa asisti.

Ushirikiano wake na Son Heungmin umeifanya Tottenham kuwa na msimu mzuri. Upande wa Aguero, ameshafunga mabao 256 katika mechi 378 alichoichezea timu hiyo.

Aguero

Akiwa na umri wa miaka 32, kwa sasa, Aguero hajapata nafasi ya kucheza mechi nyingi kutokana na majeraha kumuandama.


VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?

SOMA ZAIDI

5 Komentara

    Sawa

    Jibu

    Guardiola naona hataki masihara

    Jibu

    Pep akimchukua kane biashara imeisha

    Jibu

    Kane mwaka wake huu

    Jibu

    Maamuzi yake binafsi Kane

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.