Serikali Ya Ingilia Kati Ishu Ya Molinga.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe amesema kuwa alishangaa kuona mchezo wa JKT Tanzania, David Molinga hayupo ndani ya kikosi cha kwanza kilichoanza.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Juni 17, JKT Tanzania ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na kwenye mchezo huo David Molinga aliwekwa benchi.
Mwakyembe amesema:”Unajua timu za jeshi hazina mapumziko, wao kipindi cha Corona hakuna Corona lazima wawe fiti kwa kufanya mazoezi sasa nilishangaa nilipoona kikosi cha Yanga hakina Molinga.
“Niliwauliza wale ambao nilikuwa nao, jamani mbona Molinga hapa simuoni akianza ila baadaye kidogo nilimuona akiingia, wale ni wanajeshi lazima kikosi kitakachopambana nao kiwe na nguvu muda wote,” amesema.
Yanga wapo katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania wakiwa na alama 56 nyuma ya Azam wenye alama 58 wakati Simba wakiwa kileleni wakiwa wamejikusanyia alama 75

52 Komentara

    Huyu nae waziri wetu anatuchanga sanaa Kama vipi aruhisu tu , Timu nzima hata ikisajili wachezaji wa kigeni sawa tu

    Jibu

    Harrison Mwakyembe Anazingua#Meridianbettz

    Jibu

    Kwan lazima aanze?! Kocha ndo anajua timu ipo vipi na ni mchezaji gani aanze nani wakuingia substitute!

    Jibu

    Sasa uyu muheshimiwa nae anataka kutuchanganya sisi kwani ata mtu akiwepo lazima acheze??

    Jibu

    Kwani lazima anzee kocha ndio anajua kikosi chake kakipanga vipi kwaiyo huyo mwakembe anazingua

    Jibu

    Mmmh sielew

    Jibu

    Kwani kuna tatizo..bench lazima awepo kama hajapangwa kucheza

    Jibu

    Inaelekea mwakyembe anamkubali sana molinga

    Jibu

    Mimi ninavyojua kocha ndo anayepanga nan acheze nan asicheze sasa yeye mh na mambo ayo wapi na wapi

    Jibu

    Nijambo jema Kama wameingilia

    Jibu

    Duh ina maana Waziri Mwakyembe anamuona Molinga jembe? Kocha ni mwamuzi wa mwisho kuamua nani acheze na nani asicheze. Molinga hana kiwango chochote cha maana kubadili matokeo pale Yanga inapozidiwa#meridianbettz

    Jibu

    Jamani tuwaachie wenyewe #meridianbettz

    Jibu

    Ina maana mwakyembe anamuona molinge ni kinara?

    Jibu

    Sio kwamba yanga wanamtegemea sana molinga kila mtu anauwezo wa kucheza pati yyt

    Jibu

    Mwakiyembe anatuzingua bhuanaa

    Jibu

    Hapo ukiangalia mwakyembe anamuona molinge ni kinara#meridiaanbettz

    Jibu

    Kocha ni mwamuzi wa mwisho kuamua nani acheze na nani asicheze. Molinga hana kiwango chochote cha maana kubadili matokeo pale Yanga inapozidiwa#meridianbettz

    Jibu

    Serikali tuliendi wachieni wanyewe.

    Jibu

    Kocha ndo anajua kwa nn hakuanza kucheza

    Jibu

    Mambo ya ngoswe tumuachie ngoswe

    Jibu

    Wazir mwakyembe inaonekana ana mpenda sana molinga kumuamin mno kukosa kuanza ndio sabab ya yeye kuulizia kua yupo au hayupo mm nilijua labda hata kusafir na timu kumbe ameanzia sub kila kitu mchezaj yupi aanza nan asubir n maamuz ya kocha

    Jibu

    Waziri mwakyembe labda alibeti kuwa molinga ataanza kwenye game hiyo mimi sio kama kunakosa hapo maana haukuanza katika mchezo huo kwa sababu ya mfumo wa kocha ila baadae alicheza so hakuna ubaya hapo

    Jibu

    Molinga tena! Asante kwa makala nzuri ya kusisimua #meridianbettz

    Jibu

    Mambo ya ngoswe tumuachie ngoswe

    Jibu

    Molinga jembe

    Jibu

    Mtazamo wa waziri wa michezo sio mbaya ila tunabaki kusema mwalimu ndo kila kitu hatujajua alikua anamipango gani wa kumuweka bench

    Jibu

    Molinga alizingua sana mechi dhidi ya jkt kiukwel mapaka waziri mwakyembe kuongelea Hilo swala ni Jambo ambalo sio zur
    # meridianbet

    Jibu

    Naona mwakyembe jicho lake linamwangalia Sana molinga.

    Jibu

    Maoni:Kocha ndio alie panga kikoss nani aanze nanani akae benchi labda muheshimiwa alizoea umuona molinga kikosi cha kwanza ndio maana alishangaa kuto kumuona!

    Jibu

    Papa molinga a.k.a falcao mutu ya kucheka na nyavu suala hlo limefikah sehem husikah na Iman litapata majibu mazur thnks meridian bet kwa update

    Jibu

    Molinga hana ubora wowote pale yanga wamuache kocha atoe maamuzi yake

    Jibu

    Itakuwa waziri anampenda molinga ndomaana anaongea hivi

    Jibu

    Kuna wakati unaweza sema wanamuonea David Molinga lakini nimekuja kufahamu mapungufu mengi anayoyaonyesha Moringa ndani ya kikosi cha yanga, Umakini wake umekuwa ndio chanzo kikubwa cha kupigwa benchi mara kwa mara, Pia ni vizuri akafanyia kazi ya kutengeneza fitness yake ili aonyeshe makali yake zaidi.

    Jibu

    wazir yeye abaki na siasa tu

    Jibu

    Molinga galasa tu

    Jibu

    Mbona Mambo yanakuwa makubwa

    Jibu

    Dah inamaana waziri mwakyembe kamuona molinga jembe? Molinga hana kiwango chochote cha maana

    Jibu

    Bora hvyo tu

    Jibu

    Ukiona ivo ndo furaha yake akimuona anacheza anamfurahia ndo maana akaingilia kati.

    Jibu

    Mahaba ya waziri sasa hayo

    Jibu

    Duuh hii ni balaa

    Jibu

    Ishakua tabu

    Jibu

    Daaaah ishakua balaa

    Jibu

    Kocha ndo anapanga wachezaji

    Jibu

    Tumwachie wenyewe watamalizana

    Jibu

    Ni mtazamo wake ila kocha nae anapipango yake kwenye kikosi nani aanze

    Jibu

    Duh!

    Jibu

    Ni mtazamo wake ila kocha anamaamuzi yake na katika vita unatakiwa upambane sio kukaa nyuma bila sababu maalumu

    Jibu

    Duuuh noma sana

    Jibu

    Hiyo ni kazi ya kocha

    Jibu

    Ahsante kwa taarifa

    Jibu

    Ni wajibu wao wizara ya michezo kuingilia kati jambo kama hili

    Jibu

Acha ujumbe