UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa ripoti ya usajili amayo inatumika kwa sasa ni ileiliyoachwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo Pablo Franco raia wa Hispania.

Pablo alikuwa ndani ya Simba msimu wa 2021/22 alipobeba mikoba ya Didier Gomes alichimbishwa hapo baada ya kushindwa kutimiza makubaliano yalikuwa kwenye mkataba na mchezo wake wa mwisho ilikuwa ni Mei 28.

Katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho hatua ya nusu fainali Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mtupiaji akiwa ni Feisal Salum aliyemtungua Aishi Manula kwa pasi ya Salum Aboubhakari,’Sure Boy’.

Barbara Gonzalez,Mtendaji Mkuu wa Simba amesema kuwa wanatumia ripoti ya Pablo kufanya usajili pamoja na kushauriana na kocha mpya wa sasa ambaye ni Zoran Maki.

“Katika usajili ambao tunafanya tunatumia ripoti ya Pablo,(Franco) ambaye alitupatia pamoja na kuangalia pale ambapo kulikuwa na mapungufu kwa kushirikiana na kocha wa sasa,(Maki) ili kuwa na timu imara zaidi,” .

Pablo Franco Simba
Pablo FrancoSimba imewatambulisha wazawa wawili ambao ni Nassoro Kapama na Habib Kyombo wengine ambao ni wachezaji wakigeni ni Victor Ackpan,Moses Phiri na Augustino Okra wapo kambini nchini Misri.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa