ABDUL Sopu ndiye nyota wa mchezo wa leo dhidi ya Somalia baada ya kuifungia timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwenye mchezo wa kutafuta nafasi ya kufuzu fainali za CHAN uliomalizika kwa bao 1-0.

Bao hilo limefungwa kipindi cha pili cha mchezo huo dakika ya 46 baada ya Kibwana Shomary kumpa pasi Sopu ambaye alifunga bao hilo.

Mchezo huo umepigwa kwenye Uwanja wa Mkapa ukiwa ni mchezo wa kwanza kabla ya ule wa marudiano utakaopigwa Julai 30 mwaka huu.

Katika mchezo huo Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen alifanya baadhi ya Mabadiliko ambapo aliwatoa Aishi Manula, Abdul Sopu na George Mpole huku wakiingia Farid Mussa, Relliants Lusajo na Abutwalib Mshery.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa