KIUNGO wa Yanga na mchezaji bora wa ligi kuu Bara kwa msimu uliopita, Yannick Bangala amesema kuwa anakuja kivingine kwa kutoangalia kile alichopata msimu uliopita.
Bangala
Bangala
Bangala alikuwa sehemu ya mafanikio ya Yanga msimu uliopita ambapo alibeba mataji matatu ambayo ni Ngao ya jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam.

Akizungumzia hilo, Yannick amesema kuwa “Msimu uliopita nimefanikiwa kupata mafanikio mengi haswa ya timu yangu lakini bila kusahau yangu binafsi. Hii siyo kipaumbele changu kuelekea msimu ujao ambapo naamini natakiwa kuanza upya.
Bangala

“Natamani kuona napata mafanikio mengine mapya hivyo sidhani kama nikicheza kwa kuringia mafanikio ya msimu uliopita nitaweza kufanikiwa, lazima kupambana zaidi ya msimu uliopita.”

Kwa Taarifa Zaidi Zinahusu Michezo na Uchambuzi Bofya hapa Chini 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa