Straika Azam kuikosa KMC

STRAIKA wa Azam FC, Abdul Sopu ataukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC kutokana na majeraha ya mguu aliyonayo.
Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kupigwa Oktoba 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

Akizungumzia maandalizi ya timu yao, Ofisa Habari wa muda wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kikosi chao tayari kimeanza maandalizi ya kujiandaa na mchezo huo ujao.

“Kikosi tayari kimeanza maandalizi ya mchezo ujao wa ligi dhidi ya KMC ambapo tutakuwa ugenini na macho yetu na masikio yanauangalia mchezo huo muhimu kwetu.

“Tutawakosa nyota wetu wawili wenye majeraha ambao ni Abdul Sopu na Pape Maliku ambaye yeye tayari ameanza mazoezi mepesi.

“Sopu alipata majeraha ya mguu na hivi sasa yupo kwenye hospitali moja hapa Dar kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kugundua ukubwa wa jeraha lake hivyo tutamkosa kwenye mchezo ujao.”

Straika Mtibwa afungua akaunti ya mabao

STRAIKA wa Mtibwa Sugar, Charles Ilanfya amefungua akaunti yake ya mabao msimu huu dhidi ya Singida Big Stars.

Nyota huyo tangu kuanza kwa msimu huu hajafunga bao lolote ambapo jana jumanne alifanikiwa kuipatia timu yake bao la ushindi ambapo mchezo ulimalizika kwa bao 1-0.

Ilanfya alijiunga na Mtibwa Sugar akitokea KMC baada ya kutolewa kwa mkopo akitokea Simba.

Mtibwa Sugar kwa sasa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi nane.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.