Kocha Mserbia Ampa Mbinu Nabi

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa kikosi cha Yanga, Kostadin Papic amempa mbinu kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi kuwachezesha wazawa kuliko nyota wa kigeni.

Kikosi cha Yanga tayari kimeanza maandalizi ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba, Oktoba 23 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumzia Dabi hiyo ya Kariakoo, Papic amesema mchezo huo utakuwa mgumu lakini timu bora ndio itakayopata matokeo.

“Safari hii nitashuhudia mchezo huo kwenye TV sitoenda uwanjani, naamini timu bora ndio itapata ushindi kwani sio mzuri sana kutabiri.

“Ningependa kumshauri kocha Nabi achezeshe sana wachezaji wazawa kuliko wale wa kigeni kwenye mchezo huo wa dabi.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.