Tetesi zinasema, Klabu ya Borussia Dortmund inaamini kuwa mchezaji raia wa Norway, Erling Braut Haaland atasajiliwa na Manchester City kwenye kipindi cha kiangazi dirisha dogo litakapofunguliwa.
Alvaro Morata, 29 huenda akasitisha mkataba wa mkopo ndani ya klabu ya Juventus na kujiunga na Barcelona. Massimiliano Allegri ameonesha kutokuwa tayari kumuachia mchezaji huyo mpaka pale atakapopata mtu wa kurithi nafasi yake.
Tetesi zinasema, klabu ya Lazio imeonesha nia yake ya kumchukua kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga, lakini mshahara wake wa pauni 170,000 kwa wiki ndio unaonekana kuwa kikwazo.

Beki wa Marseille Boubacar Kamara anataka mkataba wa pauni 150,000 kwa wiki kutoka kwa klabu yake msimu ujao,hii ni baada ya West Ham kujiunga na Newcastle kupata saini ya Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22.
Barcelona imeanza kumwinda winga wa Wolves, Adama Traore, 25, ikiwa kiungo Mfaransa Ousmane Dembele, 24, ataondoka na kutoa ushindani kwa Tottenham katika majaribio yao ya kumsajili Mhispania huyo.
Tetesi zinasema, Mshambulizi wa Fiorentina na Serbia, Dusan Vlahovic, 21, yuko tayari kusubiri hadi msimu wa majira ya joto, kuanza mipango ya kuhama na sio kuharakisha kuhama Januari.
Beki wa Manchester United na Ivory Coast Eric Bailly, 27, anawaniwa na AC Milan wanaotafuta mbadala wa beki wa kati wa Denmark Simon Kjaer, 32, ambaye ni majeruhi.

Tetesi zinasema, Birmingham City wameanza mipango ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Manchester United raia wa Ivory Coast Amad Diallo, 19,
Tetesi zinasema, Aston Villa, Crystal Palace, Newcastle na West Ham zimeonesha nia ya kumsajili Msenegali, 21, Bamba Dieng wa Marseille.
Aston Villa wanavutiwa na kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma, ila kocha Graham Potter anasema Seagulls hawatomuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


