Vinicius Alivyosajiliwa Madrid!

Juni Calafat ndiye mtu aliyekuwa nyuma ya pazia juu ya sajili za Real Madrid huko Amerika Kusini, na haswa huko Brazil. Mwaka 2017, kwa mujibu wa Marca, alikutana na Vinicius Juniour akiwa na umri wa miaka 16, kwa mara ya kwanza kabisa huko Rio de Janeiro, alipokuwa Flamengo.

Florentino Perez alikuwa amempa Calafat jukumu la kumtafuta Lionel Messi mpya.

Calafat alisafiri hadi Brazil zaidi ya mara kumi kukutana na Vinicius na kumshawishi kusaini Real Madrid, ​​ambao pia walivutiwa na kijana huyo. Wawili hao waliunda uhusiano ambao unaendelea hadi leo ni marafiki wazuri.

Vinicius JuniorVinicius Junior

Calafat alihaha wakati Vinicius akihangaika kujitafuta misimu yake michache ya kwanza pale Santiago Bernabeu, lakini anafurahia hali yake hivi sasa. Mbrazil huyo amechangia mabao 12 na asisti saba katika michezo 22 ya mashindano yote msimu huu.

Ukiachana na Vinicius, Calafat pia ndiye aliyekuwa nyuma ya usajili wa Eder Militao na Rodrygo, ambao wanaendelea vizuri siku za hivi karibuni. Aliaminiwa vyema huko Madrid, alipoajiriwa kama skauti wa Amerika Kusini mnamo 2013 kabla ya kupandishwa cheo hadi katika wadhifa kama Skauti Mkuu miaka miwili baadaye.


 

AGENT JANE BLONDE AMEREJEA MSIMU WA SIKUKUU.

Unaweza kujishindia mamilioni katika kasino yako pendwa ya meridianbettz, mchezo wa Agent Jane Blonde Return ni moja ya michezo inayopendwa kwasasa huku ikiwafanya wachezaji kuwa mamilionea kila siku. Unasubiri nini! ungana na Agent Jane Blonde akufanye milionea.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.