Barcelona chini ya Xavi itasafiri kwenda Pamplona kumenyana na Osasuna kwenye Uwanja wa El Sadar kwenye La Liga. Ni mechi ngumu kwa Barcelona ambao wanaonekana wako katika hali mbaya, Osasuna ni timu ngumu kucheza katika nyakati bora hasa wakiwa El Sadar.
Osasuna hawajapoteza tangu tarehe 20 Novemba, walipoangukia pua kwa bao moja kwa mabingwa watetezi Atletico Madrid. Watafurahia fursa ya kuwalaza njaa timu Barcelona.

Kipindi cha fungate cha Xavi kimekamilika pale Camp Nou, na sasa ni kazi kazi. Xavi amebainisha mipango ya kuboresha kikosi chake kwenye dirisha lijalo sokoni.
“Tunaifanyia kazi, huo ndio ukweli, Kuna uaminifu mkubwa na tulikuwa na mkutano wenye tija. Nilikuwa wazi juu ya kile ninachoamini, ninachotaka na kile ninachohitaji. Inabidi tutafute suluhu za kuboresha timu na kuboresha kikosi.”
“Ninaelewa hali ya klabu kutokana na bili ya mishahara na vikwazo vinavyoweka, lakini tunapaswa kuboresha kikosi chetu kulingana na uwezekano tulionao.”
Unaweza kujishindia mamilioni katika kasino yako pendwa ya meridianbettz, mchezo wa Agent Jane Blonde Return ni moja ya michezo inayopendwa kwasasa huku ikiwafanya wachezaji kuwa mamilionea kila siku. Unasubiri nini! ungana na Agent Jane Blonde akufanye milionea.
CHEZA HAPA


