Kocha wa klabu ya Fc Barcelona Xavi Hernandez ameoneshwa kusikitishwa na droo ya michuano ya Uefa Europa League, Iliyochezeshwa jana na wababe hao wa Catalans kupangwa na klabu ya Manchester United kutoka nchini Uingereza.

Klabu ya Barcelona wanatolewa kwenye ligi ya mabingwa ulaya na kushuka kwenye michuano ya Europa ikiwa ni mara ya pili baada ya msimu uliomalizika pia kushindwa kufuzu hatua ya 16 bora.xaviKlabu ya Barcelona chini ya Xavi msimu uliomalizika walitolewa na klabu ya Einchracht Frankfurt kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Europe League, Ndipo kocha wa klabu hiyo anaona mwaka huu pia wamekua wenye bahati mbaya kupangwa na klabu ya Man United.

Kocha huyo anaamini wanahitaji kupambana na kuonesha ubora wa hali ya juu kutokana na mpinzani ambae wamepangwa nae ambae ni klabu ya Manchester United chini ya kocha Erik Ten Haag.

Klabu ya Barcelona mara ya mwisho kukutana na klabu ya Manchester United ilikua hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ulaya msimu wa 2018/19, Ambapo Barca waliitoa Man United kwenye michuano hiyo. xaviMchezo mwingine ambapo kocha Xavi alikua pia mchezaji ilikua fainali ya ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2011 ambapo Barcelona walifanikiwa kushinda mabao matatu kwa moja mchezo uliopigwa katika dimba la Wembley.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa