Fainali bora kuwai kutokea tangu kuanzishwa kwa kombe la Azam Confederation Cup ni mchezo wa leo kati ya Yanga SC dhidi ya Coastal Union FC ambapo kiwanja cha sheikh Amri Abeid kweli nyasi na nyavu ziliwaka moto.

Coastal Union FC mapema kwenye dakika ya 13 kupitia kwa mchezaji wake Abdul Sopu, alifanikiwa kucheka na nyavu za Yanga na kupelekea kipindi cha kwanza ubao kusomeka 1-0. Baada ya kipindi kuanza cha kiungo fundi kutoka kutoka zanzibar Feisal Salumu dakika ya 56 aliwainua wana Yanga kwa kusawazisha na kufanya mchezo kuwa 1-1.

Yanga SC

Dakika ya 82 makambo anapelekwa tena furaha kwa upande wa Yanga kwa kufunga goli safi, kabla ya Abdul Sopu kuzima furaha ya wananchi kwenye dakika ya 88 na kufanya mchezo umalizike kwa goli 2-2.

Baada ya mchezo kwenda Extra time ya dakika 30, ndani ya dakika 8 tu Abdul Sopu alipeleka furaha kwa upande wa Coastal Union, kabla ya Denis Nkane kufanya mchezo kuisha kwa sare na mchezo kwenda hatua ya matuta, na Yanga SC kufanikiwa kushinda penati nne huku Coastal Union wakipata penati moja tu na ubao kuisha kwa penati 4-1.

Hongera kwa makocha wote wawili Nabi na Mgunda kimbinu wametupa mechi tamu sana, wakakabidhi kwa wachezaji wao ambao kwa ukubwa sana wakatekeleza kwa ufanisi.

Asante kwa Yanga SC na Coastal Union FC kwa kuutendea haki mchezo wa fainali.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa