Klabu ya Newcastle United imefanikisha uasajili wa Sven Botman kutoka Lille ya Ufaransa kwa dau linaloripotiwa kufika £35m.

Newcastle wanaendelea kukisuka kikosi chao kulekea msimu mpya wa Premier League na usajili wa Botman ni moja ya sajili ghali kwa klabu hiyo baada ya kuwasijili Bruno na Joelinton kwa pauni milioni 40 kila mmoja.

Akiwa na Lille Botman alifanikiwa kutwaa taji la Ligue 1 vilevile aliwahi kupita katika klabu ya Ajax lakini hakufanikiwa kucheza katika timu ya wakubwa.

Kocha wa Newcastle United Howe alisema: “Ninafuraha Sven amejiunga nasi, ni mzuri sana kiujuzi, kimwili na mwenye tabia ya kupambana.

“Akiwa na umri wa miaka 22 tayari amecheza na timu kubwa na ataendelea kukua akiwa na timu hii.

Newcastle wanatarajia kuanza msimu mpya wa EPL kwa kumenyana na Nottingham Forest wakiwa nyumbani tarehe 6 mwezi wa nane.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa