Agosto Kutua Siku ya Mechi Kijeshi Kuwakabili Simba kwa Mkapa

TAARIFA kutoka kwenye chanzo cha kuaminika ndani ya Simba kimefunguka kuwa, kuna uwezekano mkubwa Premiero de Agosto wakatua Dar siku ya Jumapili asubuhi wakiwa na ndege ya kijeshi na kisha jioni wakaingia uwanjani kucheza na Simba.

Kiongozi huyo alidai kuwa do Agosto wamepewa kibali cha kutua nchini kwa masaa 24 na baada ya mechi yao na Simba hawatakuwa na la ziada zaidi ya kupanda pipa lao na kurejea Luanda Angola kusubiri ratiba zingine za mechi zilizopo mbele yao.

“Agosto ni timu ambayo inamilikiwa na jeshi na ndiyo maana kiongozi huyo alidai imekuwa rahisi kwao kupata kibali cha kutua nchini kwa usafiri huo. Wamepewa masaa 24 tu ya kuwepo hapa nchini na ndege yao na hivyo basi mechi ikiisha tu wataondoka zao,” alisema mtu huyo.

Alipotafutwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally ili kujua kama ni kweli wana taarifa za wapinzani wao kutua nchini kwa staili hiyo alidai kuwa taarifa hiyo hana, anachojua yeye Agosto watatua nchini leo Ijumaa.

“Kwa taarifa ambayo nipo nayo ni kwamba Agosto watatua hapa Dar siku ya Ijumaa (leo), watapata muda wa kupumzika na kufanya mazoezi kabla ya Jumapili kusubiri kunyolewa tena na mnyama Simba,” alisema.

Agosto wana deni la mabao 3-1 waliyofungwa kwenye mechi ya kwanza. Hivyo ili wasonge mbele wanatakiwa kushinda mabao 4-0. Mshindi wa jumla atatinga kwenye makundi moja kwa moja na atakayefungwa au kutolewa atakwenda kucheza shirikisho.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.