Kocha Mkuu wa Nyasa Big Bullets Calisto Pasuwa alisema kuwa, sababu kubwa ya timu yake kupoteza mchezo wao ya mkondo wa kwanza kwa bao 2 kwa 0 dhidi ya miamba wa Tanzania, Simba SC ni kwa sababu waliwaheshimu sana wapinzani wao.
Pasuwa aliyasema hayo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchezo wao huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL na ndipo alipoyasema hayo.
“Tuliwapa Simba SC heshima kubwa sana kwenye kipindi cha kwanza, kitu ambacho kilikuwa ni sababu ya kupoteza mechi tukiwa nyumbani. Haitakuwa rahisi kwetu tukiwa Tanzania” Alisema Pasuwa.
Mabingwa hao wa Malawi, walipoteza mchezo wao kwa goli 2 kwa 0 wakiwa nyumbani dhidi ya Wekundi wa Msimbazi kutoka Tanzania, Magoli yakifungwa kipindi cha kwanza na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia Moses Phiri “MP” Kamanda, kwa mtindo wa Acrobatic baada ya kupokea Pasi nzuri ya kichwa kutoka kwa Kibu Denis.
Goli la pili lilifungwa na Nahodha John Bocco baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mwamba wa Lusaka Clatous Chama.