ALI KAMWE ATOA NENO LA SHUKRANI KWA MASHABIKI

OFISA Habari wa Klabu ya Yanga Ali Kamwe amefurahishwa na Kasi ya Mashabiki wa Klabu hiyo kwa nguvu wanayoionesha kwenye kujiandikisha Ili kupata kadi za uanachama.

Ali Kamwe amewapongeza mashabiki hao Kwa kusema: “Nimefurahishwa sana na Muamko mkubwa wa Mashabiki wa Yanga tangu Jana wakitaka Kulipia Kadi zao za Uwanachama. Safi sana Wananchi.

“Tulipotembelea Al Ahly Tulipata Elimu nzuri jinsi wenzetu wanavyotumia vyema Mfumo wao wa Wanachama kuendesha Klabu yao.ali kamwe“Sasa Hivi Ahly wana mpaka kadi ya Mwanachama wa Maisha ambayo Gharama yake ni Dola 40,000. zaidi ya Milioni 100 kwa Fedha za Kitanzania.

“Kadi hii imeweza kuwaingizia kiasi cha Bilioni 200 Hadi wakati ule sisi Tunakwenda.

“Hapa huwezi kuwasikia Ahly wakiumiza kichwa kwenye kutaka kujenga Timu bora. Watasajili Yoyote wanayemtaka ili Wanachama wao wafurahi.

“Sisi Yanga Tayari Tuna Mfumo Bora zaidi wa Usajili wa Wanachama kwa Afrika Mashariki na Kati. HI IKAWE SILAHA YETU YA MAFANIKIO.

“Hapa Tunapokwenda kwenye Sherehe za Ubingwa Jumamosi, Kila Mwanayanga Ahakikishe analipia Ada Yake ya Mwaka mwingine ili Mwakani In Shaa Allah Tufurahi Tena.

“Hapa Tunapokwenda kuingia katika kipindi cha Usajili, Kila Mwanachama ahakikishe Mwaka mpya wa Fedha wa Klabu yetu, unaoanza 1/7/2024. Tuhakikishe WOTE tunalipia Ada za mwaka mwingine Ili tufanikishe Mambo Makubwa mawili.

1: Tubakize Our Best Players kwenye Kikosi chetu
2: Tushushe Majembe Mapya ya kuipa nguvu zaidi Yanga Yetu kwenye CAF CHAMPIONS LEAGUE.ali kamwe“Hii Ikawe Dira yetu na Nguvu yetu kwa sasa. Tukatae Propaganda na Uongo uongo wa kipuuzi. Zitaturudisha kwenye kuona Nafasi ya 2 kwenye Msimamo nacho ni kitu cha kutolea jasho kukipata TUSHAVUKA HUKO” Alisema Ali Kamwe

Mfumo Tunao, Mashabiki Tupo. Tulipie Ada zetu sasa kwa ajili ya Yanga.

“Karibuni kwenye PARTY LA KIBINGWA JUMAMOSI WANANCHI.”

Acha ujumbe