STEPHEN Aziz Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga amepindua Meza ya vita ya ufungaji bora mbele ya Feisal Salum baada ya kufunga mabao mawili dhidi ya Dodoma Jiji na kufikisha mabao 17 akiwa namba moja chati ya ufungaji hapo Jana.
Aziz Ki amefunga mabao mawili wakati Jamhuri, Dodoma Jiji wakifa 4-0 kwenye mchezo ambao Yanga waliwapa nafasi ya kuanza wachezaji wengi ambao uwa hawapati nafasi ya kuanza.Dakika ya 10 Clement Mzize alianza kufunga bao la kuongoza, Aziz Ki alipachika bao kwa mkwaju wa penalti dakika ya 45+4 ni yeye mwenyewe aliisababisha penalti hiyo.
Kipindi cha pili Maxi Nzengeli alipachika bao la nne dakika ya 78 ikiwa ni baada ya kushuhudia bao 17 la Aziz alilofunga dakika ya 50 akitumia pasi ya Mzize.
Kwa Mantiki hiyo Sasa, Feisal ana kibarua Cha kufunga mabao mawili kwenye mechi mbili zilizobakia Ili kuweza kuwa mfungaji Bora. Kwa kuwa Kwa Sasa ana mabao 16.Lakini wakati huo huo akiomba Dua Kwa Azizi Ki naye apate ukame wa kufunga kwenye mechi mbili pia ambazo zimebakia.
Aziz Ki amefunga mabao 17 na kutoa Assist 8, huku Feisal akiwa na mabao 16 na Assist 7. Moto unawaka kweli kweli.