Aziz Ki, amfungua mdomo Eng. Hersi

BAADA ya kuufunga mwaka 2022 kwa kishindo cha ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo wao wa kimataifa wa Burkina Faso, Stephanie Aziz Ki, Rais wa Yanga, Hersi Said amefunguka kuwa ushindi huo unatuma ujumbe mzito kuwa kasi waliyonayo wamejipanga kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Yanga Juzi Jumamosi walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo bao pekee lilifungwa na Aziz Ki.

Aziz Ki, amfungua mdomo Eng. Hersi

Ushindi huo umewafanya Yanga kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa tofauti ya pointi sita baada ya kufikisha pointi 50 katika michezo yao 19 waliyocheza mpaka sasa.

Aziz Ki, amfungua mdomo Eng. Hersi
Akizungumzia mafanikio yao kwa mwaka 2022, Hersi alisema: “Mwaka 2022 ulikuwa wenye mafanikio mengi kwetu ikiwemo kutwaa mataji matatu ndani ya msimu wa 2021/ 2022, sambamba na hilo Yanga msimu huu iliuanza mwaka vizuri na kushinda taji la Ngao ya Jamii kwenye mchezo wa ufunguzi wa msimu wa 2022/23.

“Pamoja na hayo tumefuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, na tunaendelea kuongoza msimamo wa ligi kwa tofauti ua pointi sita, ni wazi hii inatuweka katika mazingira mazuri ya kuhakikisha tunatimiza malengo yetu ya kutetea mataji yetu ya mashindano ya ndani na kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ya kimataifa.”

Acha ujumbe