Kocha wa Simba Abdelhack Benchikha, amesema kuwa haitakuwa rahisi kucheza na Jwaneng Galaxy kwa kuwa mara zote huwa hawabariki.
“Galaxy sio timu rahisi ni kama jeshi lisilotabirika, hakuna aliyedhani kama ingeifunga Wydad Casablanca nchini Morocco kwenye mchezo wa kwanza wa makundi.“Hata hapa Simba rekodi zinaonyesha wamewahi kushtua kwa kushinda hapa, nadhani mashabiki na hata wao wachezaji wanalijua hili na tayari nimeshakaa kikao na wachezaji na kuwakumbusha.
Kocha Benchikha alisema“Kwenye soka mambo ya kushtua kama haya huwa yanatokea, sitaki historia hii ijirudie hapa chini yangu, nimezungumza nao tukiwa kule ugenini juzi nadhani kila mtu ataelewa tulizungumza nini.
“Tunatakiwa kujipanga na vita nzito ya mchezo huu, nawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi kuwapa hamasa wachezaji wao wakiwa vitani ndio kitu pekee tunahitaji kutoka kwao,”“Ili kushinda tunahitaji kufunga mabao ya kutosha lakini pia kujilinda vizuri lakini kule mbele bado hatujawa imara zaidi tutawaongezea wachezaji mbinu za kutengeneza nafasi na kuzitumia kwenye hizi siku tutakazokuwa kambini” Alisema Benchikha