RAISI BFT ATEMBELEA KAMBI YA NGUMI

Raisi wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) Ndg. Lukelo Willilo amewaongoza wajumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho kutembelea kambi ya timu ya Taifa ya ngumi iliyopo katika kituo cha shule ya Filbert Bayi, Kibaha – Pwani kujiandaa na michezo ya Afrika Accra 2023 itakayofanyika kuanzia kuanzia tarehe 8-23, March, 2024 katika Jiji la Accra, Ghana.

Katika ziara hio, kamati ya utendaji ilipata fursa ya kuzungumza na wachezaji na kuwapa hamasa na kula nao chakula cha mchana.

Timu hio inatarajiwa kuondoka tarehe 09-03-2024, itakuwa na jumla ya watu 10 ambao ni wachezaji 8 (Wanaume 6 na wanawake 2) na walimu 2.

Wachezaji hao ni:-
Wanaume:-
1. Mhina Magogo 92+
2. Abdallah Abdallah “Katoto” 51kg
3. Ezra Paul 60kg
4. Abdalah Mfaume 67kg
5. Yusuf Changalawe 81kg
6. Musa Maregesi 86kg

Wanawake:-
1. Zulfa Macho 52kg
2. Mirium Richard 48kg

Walimu:-
1. Samwel Kapungu “Batman”
2. Muhsin Mng’ola

Bondia Yusuf Changalawe ataungana na timu Ghana akitokea Milan, Italy kwenye mshindano ya kufuzu Olimpiki ya Paris 2024.

Mchezo wa ngumi utaanza rasmi siku ya tarehe 14-03-2024 huku kikao cha kamati ya ufundi na upangaji wa ratiba wa mapambano ukifanyika siku ya tarehe 13-03-2024.

Pamoja na ziara hio, kamati ya utendaji ilifanya kikao chake cha kawaida cha kikatiba kujadili mipango mbalimbali ya kiutendaji kwa ajili ya mwaka 2024

Acha ujumbe