RAIS BFT AITEMBELEA KAMBI YA TIMU YA TAIFA CAMEROON

Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Shirikisho la Ngumi Afrika AFBC Ndg. Lukelo Willilo aitembelea na kula chakula cha mchana cha pamoja na Timu ya Taifa ya Ngumi inayoshiriki mashindano ya Ubingwa wa Africa yanayofanyika Yaounde, Cameroon.RaisRais aliipongeza timu kwa kazi kubwa ya kuiwakilisha nchi vizuri na kuwapa motisha wachezaji wawili watakaopanda ulingoni katika mapambano ya nusu fainali kesho Ijumaa 4-08-2023.
Wachezaji hao ni Yusuf Changalawe atakayepambana na Nathan Landu kutoka DR Congo katika uzani wa Cruiserweight 86kg na Grace Mwakamele atakayepambana na Seynabou Ndiaye kutoka Senegal katika uzani wa Lightmidddle weight 70kg.

“Hakika mmetuheshimisha Shirikisho na Taifa kwa ujumla kwa hatua hii pamajo na uchache wa ushiriki wetu, sisi wote ni washindi” alisema Raisi Willilo.RaisTanzania ina uhakika wa kupata medali mbili mpaka sasa kutoka kwa wachezaji hao na zawadi ya pesa kati ya $5,000 mpaka $15,000 kwa kila mchezaji

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.