Dili la Willy Onana Qatar Limebuma, Hatma Yake ni Wapi?

Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Willy Onana Raia wa Cameroon yuko katika hatua za mwisho za kukamilisha dili lake la kujiunga na Al Ahli Benghazi ya Libya, baada ya dili la kujiunga na Muaither ya Qatar kubuma. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Willy Onana aliyefunga mabao manne ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita, ilielezwa angejiunga na Muaither inayoshiriki Ligi ya Qatar (Qatar Stars League) lakini inadaiwa dili hilo limekwama na sasa anajiunga na Al Ahli Benghazi ya Libya.

Willy Onana aliyefanya maandalizi ya msimu ‘Pre Season’ na Simba ikiwa jijini Ismailia Misri kabla ya kukatwa dakika za mwisho ili kumpisha kipa Moussa Camara kutoka AC Horoya aliyekuja kuchukua nafasi ya Mmorocco Ayoub Lakred aliyeumia akiwa kambini katika maandalizi ya msimu mpya.

Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

Camara alisajiliwa ili kuongeza nguvu eneo la kipa baada ya Ayoub kuumia huku viongozi wa Simba wakiwa hawana imani na makipa wengine kikosini wakiongozwa na wazawa, Hussein Abel na Ally Salim ambao wameshindwa kabisa kuonyesha ushindani.

Willy Onana aliyejiunga na Simba Julai 5, mwaka jana akitokea Rayon Sports ya Rwanda ambayo aliibuka mfungaji bora baada ya kufunga jumla ya mabao 16 na kuasisti mengine matano, alikatwa ili kukidhi kigezo cha wachezaji 12 wa kigeni.

Nyota huyo mbali na kuibuka mfungaji bora akiwa na Rayon Sports ila alikuwa mchezaji bora wa msimu wa Ligi Kuu ya Rwanda (MVP), na kuwavutia mabosi wa Simba waliomsajili japo ameshindwa kuwashawishi na kupewa mkono wa kwaheri msimu uliopita.

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Acha ujumbe