Feisal Atuma Salamu Nzito

KIUNGO mpya wa Azam FC Feisal Salum amesema kuwa anafurahia kuwa kwenye changamoto mpya ndani ya Azam FC.

Ni ingizo jipya ndani ya Azam FC akitokea kikosi cha Yanga kilichotwaa ubingwa wa ligi 2022/23.FiesalFeisal alipokuwa ndani ya Yanga alikuwa anavaa jezi namba sita anaendelea kuivaa pia akiwa ndani ya Azam FC.

Kiungo Feisal Salum huyo anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaoelekea kwenye kambi Tunisia kwa maandalizi ya msimu wa 2023/24.

Nyota huyo amesema anafurahia maisha mapya na anatambua kazi itakuwa kubwa kwenye kutimiza majukumu mapya.Fiesal“Ninafurahi kuwa hapa na kupata changamoto mpya tunaamini tutafanya vizuri kufikia malengo yetu,” amesema.

Timu hiyo inatarajiwa kumenyana na Yanga kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii Agosti 9 2023 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.