KOCHA Miguel Gamondi wa Yanga unaweza kusema amejipata baada ya kubadilisha mfumo wake kutoka kutumia mabeki wa kati wawili na kuanza kutumia mabeki watatu wa kati jambo ambalo limeanza kuzaa matunda ndani ya timu hiyo.
Kitendo hiko kilionekana katika mchezo dhidi ya Al Ahly ambapo kocha Gamondi alionekana kuwatumia mabeki Ibrahim Bacca,Bakari Mwamnyeto na Dickson Job tofauti na mchezo wa kwanza dhidi ya CR Belouizdad ambapo aliwatumia Dickson Job na Ibrahim Bacca Pekee.Yanga katika mchezo huo dhidi ya Al Ahly baada ya Gamondi kubadilisha mfumo huo iliweza kumsaidia na kujikuta akitoa sare ya bao 1-1 tofauti na mchezo ambao aliwatumia mabeki wawili wa kati ambpo alipoteza kwa kufungwa mabao 3-0.
Kuelekea katika mchezo wa tatu wa makundi taarifa za ndani zinasema kuwa kocha Gamondi amenogewa na mfumo huo mpya ambao inaelezwa kuwa ataendelea kuutumia huko ugenini ncini Ghana katika mchezo dhidi ya FC Madeama.
“kocha Gamondi ameonekana kunogewa na mbinu ya kuwatumia mabeki watatu wa kati na inaweza kuendelea katika mchezo wetu unaofuata dhidi ya Madema kwa hata mazoezini amekuwa akiwachezesha pamoja mabeki hawa na kuwapa maelekezo ya kutosha,”kilisema chanzo hiko.Kwa upande wa Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe alisema kuwa “Hayo ni mammbo ya kiufundi anatakiwa kuyaelezea mwalimu kuhusu kubadili mbinu na timu itacheza vipi kwa upande wetu niweze kusema kuwa tunahitaji matokeo ya ushindi zaidi katika mchezo huu dhidi ya Madeama FC kuliko kitu chochote hivyo tunakwenda kuhakikisha kuwa tunapambana kwa kuwa sio rahisi lakini itabidi tujitahidi kwa hilo,”alisema Ally Kamwe.